DaudiPages AcademyDaudiPages

Bookshop

Books by Daudi

Available on DL Bookstore and other platforms.

Bundle offer

Get all 5 books

TZS 30,000TZS 37,995
Get all books
Geuza Wazo Lako Kuwa Kitabu

Geuza Wazo Lako Kuwa Kitabu

Daudi Lubeleje

Una wazo la kitabu lakini hujui ulianzie wapi? GEUZA WAZO LAKO KUWA KITABU ni mwongozo unaokuongoza kutoka kwenye wazo hadi kwenye kitabu kinachoweza kusomwa na kufika kwa wasomaji. Utajifunza jinsi ya kujenga wazo imara, kuwaelewa wasomaji wako, kuunda wahusika na muundo wa hadithi, kuandika kwa mtindo unaovutia, kufanya utafiti, kuhariri na kuboresha maandishi, kisha kuchagua njia sahihi ya kuchapisha na kusambaza kitabu chako. Kama unaamini una kitabu ndani yako, huu ndio mwongozo wa kuanza kukitoa kichwani na kukiweka mikononi mwa msomaji.

eBookTZS 9,999
Mbinu rahisi za kuandika kitabu

Mbinu rahisi za kuandika kitabu

Daudi Lubeleje

Aliwahi kusema Kate Grenville, mwandishi wa vitabu, kuwa;  “hakuna anayezaliwa anajua kuandika lakini ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza na kwa kadiri unavyoendelea kuandika ndivyo mchakato unavyokuwa rahisi zaidi”.  Hivyo basi, ni matumaini yangu ukimaliza kusoma kitabu hiki utaweza kuandika kitabu cha ndoto yako, lakini usisahau kunijpatia mrejesho mara uanzapo kuandika kitabu chako, nitafurahi sana!.

eBookTZS 3,999
Kutoka kuandika mpaka kuuza kitabu

Kutoka kuandika mpaka kuuza kitabu

Daudi Lubeleje

Ilikuwa ni kiu yangu ya muda mrefu kuandika kitabu kimoja ambacho mtu akikisoma atakuwa amepata vitu muhimu sana na vya msingi kwenye uandishi wa vitabu kuanzia hatua ya kuandika mpaka kuuza kitabu. Kwenye kitabu hiki nimeshughulika na mambo matatu; Ufahamu wa mbinu za kukusaidia kuandika, kutoa na kuuza kitabu chako. Uandikaje kitabu? Mchakato wa kutoa kitabu ukoje? Kitabu kinafikaje kwa wasomaji na unakiuzaje?. Unapokisoma kitabu hiki, utapata utajiri wa mbinu za kukusaidia kwenye maeneo yote haya Ufahamu wa makosa ya kuepuka. Huwezi kuepuka kosa usilolijua, hivyo nimeanza kwa kukuonesha makosa yenyewe ili uweze kuyaepuka.Kuyaepuka makosa haya itakusaidia kuufurahia uandishi wa vitabu kwa kuyachuma mafanikio yake. Kutatua makosa ambayo waandishi huwa wanakwama kupata utatuzi wake. Makosa haya hujitokeza kuanzia hatua ya kuandika mpaka kuuza kitabu. Kusoma kitabu hiki kutakupa kujua jinsi ya kutatua makosa hayo. Huishii tu kusoma kitabu. Upo huru kabisa kupata usaidizi kutoka kwangu, unapoendelea kusoma kitabu na ukaona kukwama kwenye jambo fulani, wewe nitumie meseji au nipigie, tutazungumza! Upo tayari kuanza safari nzito ya kusoma sura sita zilizoshiba? Haya anza!

eBookTZS 9,999
Uandishi wa kitabu kinachouzika

Uandishi wa kitabu kinachouzika

Daudi Lubeleje

Mwenye ndoto ya kuandika na kutoa kitabu ni wewe si mtu mwingine, mwenye ndoto ya kuuza nakala nyingi ni wewe na si mtu mwingine, na mwenye ndoto ya kuwa mwandishi aliyefanikiwa ni wewe na si mtu mwingine. Kwenye hatua yoyote uliyoko sasa; iwe kuandika, kutoa ama kuuza kitabu chako, kitabu hiki kitakuwa msaada kwako. Unapoanza kusoma kitabu hiki unakuwa umeanza safari ya siku 25 za kuwa mwandishi aliyefanikiwa bila stress. Utafanikiwa kutimiza ndoto yako ya kuandika, kutoa na kuuza kitabu chako kwa mafanikio. Msukumo wangu wa kuandika kitabu hiki ni kukushirikisha uzoefu wangu kwenye uandishi wa vitabu utakaokusaidia wewe usikwame kwenye kutimiza ndoto yako. Nimeunganisha uzoefu wangu wa kuandaa kozi za uandishi, niliyopitia kwenye kutoa vitabu vyangu na ushauri niliotoa kwa watu mbalimbali waliokuwa wamekwama hatua walizokuwa kwenye uandishi wa vitabu. Kwa kifupi, kitabu hiki kinamfaa yeyote anayetaka; Kuandika kitabu Kutoa kitabu Kuuza kitabu Ninaposema uandishi wa kitabu kinachouzika, naamanisha kuwa uandike kitabu kitakachofika mkononi mwa msomaji wako na hiyo ndiyo furaha ya mwandishi yaani kuona msomaji amesoma, amejifunza na kukifurahia kitabu. Upo tayari kuanza siku 25 za kuwa mwandishi aliyefanikiwa? Upo tayari kuandika kitabu kitakachofika kwa msomaji wako?

eBookTZS 9,999
Naandikaje kitabu?

Naandikaje kitabu?

Daudi Lubeleje

Kitabu hiki ni toleo lililoboreshwa la kitabu cha Mbinu Rahisi Za Kuandika Kitabu. Wakati nilipotoa kitabu cha Mbinu Rahisi Za Kuandika Kitabu nililenga kuwasaidia watu wanaotaka kuingia kwenye uandishi wa vitabu lakini hawana watu wa kushika mkono ili kufanikisha ndoto zao. Lengo bado ni lile lile isipokuwa nimeboresha zaidi na kufanya marekebisho fulani fulani baada ya kupokea maoni kutoka kwa wasomaji wengi waliosoma kitabu. Katika toleo hilo jipya, nimeongeza vitu vingi ambavyo naamini, unapokisoma kitabu hiki utatoka ukiwa na nguvu mpya ya kuandika kitabu chako na hatimaye kutimiza ndoto yako ya kuwa mwandishi wa kitabu. Naandikaje kitabu? Ni swali ambalo nimejibu katika kurasa zinazofuata. Mimi naamini, kuandika kitabu ni ujuzi ambao kila mtu anawez kujifunza Anza kusoma!

eBookTZS 3,999TZS 4,999